Waumini
wa kanisa la EAGT Pangani mjini mnamo tarehe 26Nov2017 waliamua kufanya sherehe
ndogo inayolenga kumshukuru MUNGU kwa kiongozi wao wa kanisa hilo Mch NAFTAL MSOLOKA
kuwekewa mikono kuwa mwinjilisti wa taifa.
Aawali
akitoa maelezo ya shughuli hiyo fupi Mzee wa kanisa na Katibu wa kanisa hilo Dr
Josephat Makombe amesema kanisa hilo linamuunga mkono Mch Msoloka kwa kila
atakokokwenda katika kazi ya kumtumikia MUNGU aliyemuita.
“lengo
la sherehe hii fupi ni kumshukuru MUNGU kwa mchungaji wetu kuwekewa mikono na
askofu mkuu kuwa mwinjilisti wa Taifa nasi tuko pamoja nawe katika kukuunga
mkono kila uendako kufanya kazi ya MUNGU na tunakuahidi kama kanisa tuko nyuma
yako” alisema Dr Makombe.
“kama
kanisa sasa kwa hatua uliyofikia tunakushauri uanze harakati ya kutafuta
pasport ya kusafiria kwani tunaamini kuwa sasa utakuwa na kibali cha kwenda
hata nje ya mipaka ya Tanzania na afrika
mashariki kwa ujumla na kwenye hili tuko pamoja nawe, pia tunakushauri uanze
mazoenzi ya kujifunza lugha za kigeni ili iwe rahisi katika kufanya mawasiliano
huko uendako” aliongeza Dr Makombe.
Katika
kumtakia kumtia moyo kiongozi huyo ambae ni Mwinjilisti Kitaifa kwa sasa
Vijana, kinababa, kinamama na watoto wamesema katika kipindi ambacho hatukuwepo
kanisani humo asifikirie u ya waliobaki kuwa watabakije ila ajue kuwa wako pamoja nae katika maombi muda wote ili
kufanikisha kazi ya Mungu.
Tazama
baadi ya picha kwenye tukio hilo.
Mch
Naftal Msoloka akiingia kanisani.
waumini
wa kanisa wakimlaki Mchungaji Msoloka.
Mch
Naftal Msoloka akiwa na Mkewe
Baadhi
ya waumini wa kanisa
Dada
Joyce akifungua zawadi ya mama mchungaji kwa niaba ya kanisa.
Kijana
John kisiwa akifungua zawadi ya Mchungaji kwaniaba ya kanisa.
.............................. .........
Email: panganieagt@gmail.com
tembelea Youtube chanel yetu kuona mahubiri ya Mch Naftal Msoloka kwa kuandika EAGT PANGANI.
usisahau ku-subscribe.
Sign up here with your email