Arsenal wainyuka Brighton 2-0

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesherehekea miaka 21 ya kuiongoza Arsenal kwa ushindi dhdi ya Brighton Nacho Monreal aliwaweka Arsenal kifua mbele kufuatia mkwaju aliosukuma karibu na eneo la penalti baada ya Brighton kushindwa kuondoa mpira eneo hatari. Arsenal walifunga bao la pili baada ya mapumziko kufuatia counter-attack ambayo ilikamilishwa na Alex Iwobi. Baada ya ushindi huo Arsenal sasa wako pointi moja nyuma ya mahasimu Tottenham ambao pia wako nyuma na viongozi wa ligi Manchester City.
Previous
Next Post »