Sign up here with your email
SIJAJA SIMBA KUFANYA KULETA MAAJABU
Kocha msaidizi mpya ndani ya kikosi cha Simba Masud Djuma amesema hajaenda klabuni hapo kufanya maajabu bali ni kutoa mchango wa kile alichonacho kwa kushirikiana na benchi la ufundi lililopo sasa
“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi”
Alikuwa kocha mkuu msimu uliopita wakati anaifundisha Rayon Sport ya Rwanda kabla ya mkataba wake kumalizika. Akashinda tuzo ya kocha bora wa msimu wa Azam Rwandan Premier League.
“Nilianzia chini, baafa ya kuwa kocha bora Rwanda nikasema sitaki tena kuwa kocha msaidizi ndani ya Rwanda nimekuja hapa kuwa chini ya kocha mkubwa ni kama mzazi kwangu nahitaji kujifunza kutoka kwake ili nipande.”
“Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.
“Sisi makocha ni kama mabegi, hupaswi kufungua zipu yote kwa sababu muda wowote unaweza kuondoka.