Ben pol amtabiria makubwa msaga sumu

Msanii wa Bongo Flava, Ben Pol amesema msanii Msaga Sumu atafika mbali kutokana ana uziki wake wa pekee. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kidume’ aliyomshirikisha Chidinma kutoka Nigeria ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa licha ya msanii huyo kufanya vizuri ila bado hajaeleweka iwapo ni upcoming au lah!. “Sijui kama Msaga Sumu ni upcoming au siyo lakini napenda sana muziki wake na jinsi anavyokuja, ana-flavor yake kama Dr. Remmy au sound fulani hivi ya kitofauti sana namuona atafika mbali” amesema Ben Pol. “Halafu anaweza akabadilika kila mara muda mwingine anaimba kama zilipendwa, anaimba kisengeli, kama oya oya lakini ana vitu vingi sana” ameongeza. Msaga Sumu kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mwanaume Mashine’ baada ya kufanya vizuri na ngoma Shemeji Unanitega.
Previous
Next Post »