Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Heather Nauert amezitaka penda zote kuzuia makabiliano zaidi.
Wanajeshi wa Iraq walielekea Kirkuk wiki tatu zilizopita, baada ya eneo la Kurdistan kuandaa kura ya maoni ya uhuru iliyokumbwa na utata
Lengo lao ni kuteka sehemu zilizo chini ya udhibiti wa wakurdi tangu Islamic State wadhibiti eneo hilo.
Wenyeji wa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa wakurdi ukiwemo mji wa Kirkuk, kwa wingi waliunga mkono kujitenga kutoka Iraq wakati wa kura ya tarehe 25 mwezi Septemba.
Licha ya mji wa Kirkuk kuwa nje ya eneo la Kursistan, wapigaji kura wa Kurdistan walio mjini humo waliruhusiwa kushiriki kura.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi aliitupilia mbali kura hiyo na kuitaja kuwa iliyo kinyume na katiba.
Sign up here with your email