Sign up here with your email
Lionel Messi na Christian Ronaldo ngoma droo
Barcelona imeendeleza ushindi wa asilimia 100 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitwanga Olympiacos kwa mabao 3-1,lakini kikubwa katika mechi hiyo ni pale mchezaji bora mara tano wa dunia Lionel Messi alipoweza kupachika goli lake kwa mkwaju wa faulo na kufikisha idadi ya mabao100 katika mchuano ya Ulaya.
Wakati Messi akifunga bao lake la 100 na kutoka uwanjani na furaha,Mambo yalikuwa mabaya kwa beki Gerard Pique baada ya kulambwa kadi nyekundu mapema tu katika mchezo huo.
Messi sasa anakarbia kufikia rekodi ya Chritiano Ronaldo ya kuwa mmoja kati ya wachezaji waliofikisha mabao 100 katika mashindano hayo.