Sign up here with your email
Idadi ya watoto walio na unene wa juu wa mwili yaongezeka duniani
Idadi ya watoto na vijana walio na uzito mkubwa wa mwili imeongezeka mara dufu, ikimaanisha kuwa watoto milioni 124 kote duniani ni wanene zaidi kwa mujibu wa utafiti mpya
Kulingana na jarida la Lancest idadi hiyo ndiyo kuwa zaidi ya aina yake na inaanagzia visa vya unene wa mwili kwa zaidi ya nchi 200.
Nchini Uingereza moja kati ya vijana 10 walio kati ya umri wa miaka 5 na 19 wako na unene mkubwa wa mwili
Watoto walio na unene mkubwa wa mwili wana uwezekano wa kuendelea na hali hiyo wanapokuwa watu wazima na kuwaweka katika hatari kubwa ya kiafya kwa mujibu wa wataalamu
Watafiti wanaamini kuwa kuwepo kwa vyakula vya bei ya chini vya kenenepesha ni moja ya sababu