Wizkid sio mtu wa mchezo mchezo aweka rekodi London

Staa wa Muziki kutoka Nigeria WizKid ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kujaza ukumbi wa Royal Albert Hall mjini London. Show ya WizKid ilifanyika September 29 na siku mbili kabla ya show hio tayari ticket zote za show zilikuwa zimeuzwa. Show hii ya WizKid ilirushwa Live katika kurasa ya Facebook ya WiKid na alisindikizwa na wasanii kutoka Uingereza kama Yxng Bane na kutoka Nigeria alikuwa Wande Coal, WizKid alifanya show ya Saa Moja #StandAlone na kuimba nyimbo zake zote zilizowahi kushika chati toka ameanza muziki


  Baada ya mafanikio haya Tayari mashabiki wameanza kufananisha tour ya WizKid na ya Davido ’30 billion World Tour’ ambayo pia imekuwa na mafanikio makubwa. Kwa sasa Wizkid ana furahia mafanikio ya colabo aliyopewa na Drake ya ‘One Dance’, iliyotajwa kama wimbo uliosikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Spotify September 22 na kuingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guinness Book of World Records na pia kuwa msanii kutoka Africa ambaye ambaye amesikilizwa kwenye mtandao wa Spotify mara bilioni 1,379,041,180 na kushika na #57 ya wasanii waliosikilizwa zaidi.
Previous
Next Post »