Kala jeremiah asema akiingia kwenye siasa basi atagombea u rais.

Msanii Kala Jeremiah ambaye amekuwa kifanya muziki wenye kuhamasisha sana jamii, amesema iwapo ataingia kwenye siasa ataingia kwa lengo la kuwa Rais wa nchi, na sio nafasi nyingine Kala ametoa kuli hiyo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kwamba nafasi ya hiyo ya urais ambayo ndiyo nyadhifa kubwa serikalini, ndiyo anayoikusudia kwenye maisha yake, kwani kama ni ubunge ameshafanya sana kazi za ubunge “Wengi wananishauri niingie kwenye siasa, unajua kauli ya wengi ni kauli ya Mungu, kama nitaamua kuingia kwenye siasa nafasi ya urais ndo itanifaa zaidi kwa sababu ubunge nishafanya, nilipotoa wimbo na dada yangu Nakaaya wengi walikuwa wananiita mbunge, hivyo siwezi kuingia kwenye siasa kwa kutamani kuwa mbunge, nitatamani kuwa Rais”, amesema Kala kala jeremiah kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa kijana aliomshirikisha fetty kalumba.
Previous
Next Post »