Raila Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi mkuu Kenya

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao unapangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu. Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC, muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia iliyo nzuri Awali tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi. Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4. Upinzani nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye uchaguzi mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika. Upinzani unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na kutoa muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi kufanyika kuambatana na sheria na katiba
Previous
Next Post »