Gavana wa mji wa Pennsylvania, Tom Wolf apinga hukumu ya Meek Mill

Baada ya mastaa kama JAY-Z , Dj Khaled, T.I , Rick Ross kupinga vikali hukumu ya miaka miwili mpaka minne jela kwa rapa Meek Mill, sasa Gavana wa mji wa Pennsylvania Mh Tom Wolf, amesaini Petition ya Ombi la kutaka Mahakama kutazama upya hukumu ya Meek Mill inayodaiwa kutolewa kwa UONEVU Na UBAGUZI Mkubwa huku akiomba watu waende kusaini HATI hio kwa wingi zaidi.
Ombi la Gavana Tom linasema ‘Msanii Meek Mill amekuwa kama sauti yenye nguvu kwa jamii yetu na hasa kwa vijana, amekuwa na mchango mkubwa kwa jamii na miradi tofauti kwa kujitolea muda na pesa zake mwenyewe’

Ombi hili linalofahamika kama (Petition) kwa lugha ya kingereza limewekwa mtandaoni na linahitaji kila aliyekerwa na hukumu ya Meek Mill kutoka kwa jaji Genece Brinkley kuisaini ili saini ziwe nyingi na kufanya mabadiliko ya hukumu hio. Mpaka sasa zaidi ya watu 30 wametia saini.
Previous
Next Post »