Full stori A-Z ,Alichosema Dogo Janja kuhusu,NDOA, Irene kubadili Dini, KIKI viko hapa

Haya mambo sita aliyesema Dogo Janja kuhusu ndoa yake na Irene Uwoya, Ni Kweli wamefunga NDOA Na Sio KIKI Kama ilivyoaminika mapema kama alivyothibitisha jana kwenye kipindi cha Leo Tena #CloudsFm
Dogo Janja kuhusu kabla ya ndoa>>Mwenyezi Mungu yuko mbele ya kila kitu changu ata wakati niko na Irene nilikuwa nasali Mwenyezi Mungu anipe mke bora.
Dogo Janja kuhusu kitu alichokiona kwa Irene>Nilichokiona kwa Irene Uwoya, anafaa kuwa Mama wa familia yangu, ni mwanamke ambaye nje ya ustaa wake anafaa kuwa Mama wa nyumbani kabisa
Dogo Janja kuhusu ushawishi kwa jamii>Mimi kumuowa Irene nimeishawishi jamii na vijana nao sasa wamekuwa sio waoga.
Dogo Janja kuhusu Irene Uwoya kubadili dini>Irene alibadili dini wiki tatu kabla ya kufunga ndoa
Dogo Janja kuhusu ndoa kuwa KIKI>Watu hawaamini hili tukio kuwa nimewezaje, mwisho wa siku watu watasema vitu vingi ila mimi ndiye niliyeoa na ndiye Mume
Dogo Janja kuhusu Posa >Mtu aliyepeleka posa ni Mzee Ally baba yake Madee na Sheikh aliyefungisha Ndoa ni Chande Omary Chande

Previous
Next Post »