Rapper na mtaalamu wa kuchezea pikipiki kutoka marekani
Meekmill
yupo matatani kufungwa jela kwa miaka miwili mara baada ya kukutwa na
mashtaka mawili mazito. Moja ikiwa ni kukamatwa mapema mwaka huu mwezi
March akipigana katika uwanja wa ndege wa
St. Louis, na shtaka la pili kukamatwa akiendesha chombo cha moto kwa kasi.
Mkali huyo ambae ameshawahi kutoka kimapenzi na mwanadada
Nicki Minaj
huenda akawa anakutwa na mashtaka mengi ya kuendesha pikipiki kwa kasi
kutokana na uzoefu wake mwingi wa kutumia vyombo hivyo yeye na kundi
lake.
Sign up here with your email