Mchezaji huyo wa miaka 32 kutoka Uhispania alicheza mara ya mwisho Oktoba 2016.
Alifanyiwa upasuaji kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia miezi miwili baadaye.
Lakini licha ya kufanyiwa upasuaji mara nane, kidonda chake hakikupona na badala yake alianza kuugua.
Cazorla ameambia gazeti la Marca kwamba ugonjwa huo ulikuwa "umekula" kano za kifundo cha mguu wake wa kulia.
"Sehemu ya ukubwa wa sentimita nane ilikuwa haipo," anasema.
Licha ya kutibiwa mara kadha kwa mafanikio, bado kulikuwa na wasiwasi kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Villarreal na Malaga angepoteza mguu wake kutokana na maambukizi kwenye damu yake.
Mara ya mwisho kwake kufanyiwa upasuaji sehemu hiyo ilikuwa 29 Mei.
Wakati huo madaktari walipandikiza ngozi kutoka kwa mkono wake wa kushoto - ambayo ina chale kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia.
Tangu wakati huo, Cazorla amekuwa akishiriki mazoezi na amesema anatarajia kuwa sawa kucheza mwakani.
Sign up here with your email