Aliyetekeleza shambulizi la New York afikishwa mahakamani

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamiaji kutoka nchini Uzbek anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani.
Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kuwasambazia vifaa kundi la kigaidi la Islamic State.
Akizungumzia mashataka yaliyofunguliwa kaimu mwanasheria mkuu JOON Kim amesema Saipov amefunguliwa mashitaka ya makosa mawili ya ugaidi
Shitaka la kwanza ni kutoa vifa vya kusaidia maandalizi ya shambulio la kigaidi kwa kundi la IS, na shitaka la pili kusababisha uharibifu wa magari ambayo yalisabisha vifo na majeruhi.
Naye Rais Donald Trump akionekana na baraza lake katika ikulu ya white house, amesema kuwa anatarajia kuchukua hatua za haraka dhidi ya mfumo wa uhamiaji nchini humo.
Hata hivyo Rais Trump ametaka adhabu kali kutolewa dhidi ya watu wanaobainika kujihusisha katika vitendo vya kigaidi, kama hili la New York.


Previous
Next Post »