Sign up here with your email
Rapa Meek Mill ahukumiwa kifungo cha miaka Miwili jela.
Rapa Meek Mill wa lebo ya Rick Ross ‘MMG’ amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kuvunja masharti ya mahakama ya muda wake chini ya Uangalizi wa mahakama na polisi (Probation) uliotokana na kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya pamoja na silaha kinyume cha sheria mwaka 2008.
Jaji katika Mahakama mjini Philladelphia amempa adhabu hii Meek Mill kutokana na makosa mawili makubwa Uraiani,
-Kupigana katika uwanja wa ndege wa St. Louis mwezi March mwaka huu
-Na hivi karibuni Meek alikamatwa kwa kusa la fujo, kuendesha chombo cha moto vibaya kiasi cha kuhatarisha maisha yake na ya raia wengine.