Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean

Kimbunga kikali kwa Jina Irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo takriban watu saba wameuawa. Kisiwa kidogo cha Barbuda kilisemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa himaya ya Uingereza ya St Martin imeharibiwa kabisa. Wakati huo huo upepo umetajwa kupata nguvu na kuwa vimbunga viwili. Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.
Previous
Next Post »