ARSENAL YAIYANGAMIZA CHELSEA KWA MIKWAJU YA PENALTI

Katika mchezo wa ngao ya jamii uliochezwa kati ya mafahari wawili wa London  Washika mitutu wa mji huwo Arsenal dhidi ya matajiri wa mji the blues Chelsea.Mtanange huwo umemalizika kwa chelsea kufungwa kwa njia ya mikwaju ya Penalt Nne kwa moja.Huku mlinda mlango wa chelsea Thibat Couthois akikosa mkwaju wa penalti pamoja na mshambuliaji wao mpya kutoka Real madrid alvaro morata,Shujaa wa arsenal leo alikuwa Petr Cech ambaye alicheza kwa umahiri wa hali yajuu kwa kuokoa michomo kadhaa langoni mwake.Chelsea ndio waliokuwa wakwanza kupata bao dakika ya 46 kupitia Victor Mosses huku dakika ya 80 kiungo wa chelsea pedro alilambwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwa.Bao la kusawazisha la Arsenal lilifungwa na Kolasinac mara baada ya faul ndefu huku walinzi wa chelsea walizani ameotea ndipo akaunganisha mpira huwo moja kwa moja kamabani.Penalt za arsenal leo zilifungwa na Theo walcot,Nacho monreal,Chamberlain na Olivia Geroud.Huku penalti ya chelsea ikifungwa na Cahil
 wachezaji wa arsenal wakishangilia mara baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti hii leo


Previous
Next Post »