Ronaldo alimsukuma mwamuzi Ricardo de Burgos Bergoetxea mara baada ya kumlamba kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekundu katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya Barcelona.
Pamoja na kufungiwa mechi tano pia Ronaldo amepigwa faini ya pauni 2,700 kutokana na kitendo hicho.
Kwa upande wa Kocha Mfaransa Zinedine Zidane amefunguka na kusema kwamba "Kilichoniudhi mimi siyoRonaldo kutolewa, sawa labda haikuwa penati lakini kumuonyesha kadi ni maamuzi makali".
Sign up here with your email