Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais
Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi
ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC).
Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilimtangaza
Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake
Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John
Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara
nyingine tena.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC)
ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni
uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga
kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.
Sign up here with your email