Kichuya kupaa Uarabuni

Kiungo wa Klabu ya Simba, Shiza Ramadhan Kichuya anategemewa kuachana na timu hiyo, kisha kujiunga na Waarabu wa Misri muda wowote endapo tuu dau la kushiba litakapowekwa mezani. Tetesi za taarifa kuhusu Kichuya kuondoka ndani ya Klabu hiyo bado zimekuwa uvunguni sana kwa madai kuwa Waarabu hawajafikia dau linalotakiwa ili kumtoa kiungo huyo machachari awapo uwanjani. "Kichuya kuwavutia wamisri tunalifahamu, hata hizo tetesi za kuhusu kuondoka siwezi kuzithibitisha kwani dili halijakafika mezani. Lakini pia hao Waarabu wakija na mzigo wa kutosha ambao Simba tunauhitaji tutawapatia Kichuya lakini mpaka sasa nachoweza kusema bado Kichuya ni mali ya Simba SC" ,alisema Msemaji wa Simba Haji Manara wakati akifanya mahojiano na ukurasa huu.
Previous
Next Post »