Wizkid atafutwa na Money

Msanii Gigy Money ambaye hakauki kwenye 'media' kutokana na vituko vyake, amefunguka ndoto zake za kumteka kimapenzi nyota wa Nigeria Wizkid, ambaye kwa sasa anafanya ma-collabo na wasanii kutoka Hollywood.



Gigy Money amesema ana imani ndoto yake hiyo ipo siku ataitimiza kama alivyoitimiza kwa Tekno, na lazima atawathibitishia umma kuwa ameitimiza ili asichekwe.
"Namkubali kinoma yani, ntabeba tshirt alafu ntaunganiha mapicha, ntawaambia jamani, mnakumbuka hii alishutia video fulani, hii hapa, mimi niko 'serious' na mpambano wangu nimekamilisha, mimi huwaga napenda tu kuwahakikishia lakini wao wanafikiriaga vingine, unajua ndoto siyo wote wanatimiza", alisema Gigy Money.
Gigy Money alisema hata kwa msanii Tekno alikuwa na ndoto kama hiyo na alihakikisha ameitimiza, na kuweka ushahidi mezani.
Previous
Next Post »