Katika siku ya jana Kulichezwa mchezo wa Fainali Kati ya bingwa wa Uefa Champions Leageu ambaye ni real Madrid,Na bingwa wa Europe Super league Manchester United.Mchezo huu ulichezwa Skopje Kule Macedonia,Ambapo Kocha kijana Zinedine Zidane Au kama wengi wanavyomuita Zizzou Kwa mara nyengine aliweza kukiongoza kikosi chake kuanza msimu mpya na kombe mara baada kuichapa Manchester United inayonolewa na Mreno jose Morinho.Real madrid Wakianza kwa mchezo wa taratibi katika dakika kumi na tano za kipindi cha kwanza huku Manchester united wakionekana kuanza vyema mchezo kwa mashambulizi kadhaa,Mambo yaliharibika Dakika ya 24 mara baada kijana kutoka Brazil kuwazidi ujanja walinzi wa Reds Devil na kuuweka mpira Kimiani kwa ufundi wa hali ya juu kwa kumchambua vyema mlinda lango David De Gea,Dakika ya 52 alikuwa ni Isco aliyeipatia bao la Pili REAL baada naye pia kufunga kiufundi kwa kumchambua De gea katika Angle ya Kulia.Manchester United wao walipata bao lao la kufutia machozi kupiti kwa Romelu lukaka baada kumalizia Kigongo kilichopigwa na Nemanj Matic Kumshinda mlinda lango Navas Ukamkuta Likaku na kumalizia kuweka wavuni dakika ya 62.
ISCO AKIIFUNGIA REAL MADRID BAO LA PILI KWA KUMCHAMBUA VYEMA MLINDA MLANGO DAVID DE GEA ASIJUE LA KUFANYA.
ROMERU LUKAKU AKIONEKANA MWINYE HISIA ZA USHINDI MARA BAADA KUIPATIA MANCHESTER UNITED BAO LA KUFUTIA MACHOZI DAKIKA YA 62.
ROMERO LUKAKU AKIWAHISHA MPIRA KATI MARA BAABA YA KUFUNGA.
KATIKA VIKOMBE NANE KOCHA ZIDANE AMEIBUKA NA VIKOMBE SITA
WANANDINGA WA REAL MADRID WAKISHANGILIA UBINGWA |
Sign up here with your email